• HABARI MPYA

  Wednesday, February 26, 2014

  MAN MOYES YACHAPWA 2-0 UGIRIKI

  MAMBO yamezidi kumuendea kombo kocha David Moyes baada ya kuambulia kipigo cha mabao 2-0 mjini Athens Ugiriki. Nyota wa Arsenal anayecheza kwa mkopo Olympiacos, Joel Campbell alifunga bao la pili dakika ya 55 katika ushindi huo dhidi Manchester United kwenye mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
  Campbell hakuwahi kugusa mpira The Gunners tangu aliposajiliwa mwaka 2011, lakini usiku huu alionyesha kiwango cha juu akiwa na jezi ya Olympiacos.
  Alejandro Dominguez aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 38 na sasa United inatakiwa ishinde 3-0 katika mchezo wa marudiano mjini Manchester ili kusonga mbele.
  Katika mchezo mwingine, wenyeji Zenit wamefungwa mabao 4-2 na Borrussia Dortmund. Mabao ya Dortmund yemefungwa na Mkhitaryan, Reus na Lewandowski mawili, wakati ya Zenit yamefungwa na Shatov na Hulk.
  Wa mkopo; Campbell akishangilia baada ya kuiangamiza Man United usiku huu 
  Celebration: Dominguez (centre) wheels away with his team-mates after scoring the opener in Greece
  Sherehe: Dominguez (katikati) akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la kwanzaDesperate: Moyes' last hope of silverware this season is in Europe, but they have an uphill task
  Kocha Moyes akitoa maelekezo kwa Patrice Evra
  50/50: Olympiacos' Leadro Salino (left) fights with United's Ashley Young
  Mchezaji wa Olympiacos, Leadro Salino (kushoto) akigombea mpira na Ashley Young wa United
  Not happy: Rooney discusses another matter with referee Gianluca Rocchi after the second goal
  Wayne Rooney akilalamika kwa refa Gianluca Rocchi baada ya bao la pili 
  Nowhere to be seen: United were outplayed in every area in Greece on Wednesday night
  Wachezaji wa United wakisikitika uwanjani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN MOYES YACHAPWA 2-0 UGIRIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top