• HABARI MPYA

    Friday, February 21, 2014

    UCHAGUZI TASWA MACHI 2 DAR

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    UCHAGUZI Mkuu Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TASWA, Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, fomu kwa ajili ya waombaji uongozi zinaanza kutolewa Jumatatu (Februari 24 mwaka huu) kwenye ofisi za Idara ya Habari. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.

    Wambura amesema kwamba ada kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.
    Amesema Kamati ya Uchaguzi inawahimiza wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kugombea, lakini vilevile waisome vizuri Katiba ya chama chao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UCHAGUZI TASWA MACHI 2 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top