• HABARI MPYA

    Sunday, February 23, 2014

    TWIGA STARS YAENDELEA KUJINOA KUIKABILI ZAMBIA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    TIMU ya  soka ya taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia (Shepolopolo) itakayochezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu).
    Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage na Msaidizi wake Nasra Juma inaendelea vizuri, na kwa mujibu wa programu ya benchi lao la ufundi kesho (Jumatatu), Jumanne na Jumatano itafanya mazoezi saa 10 jioni.

    Mazoezi hayo yatafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Uwanja huo ndiyo utakaotumika kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
    Shepolopolo ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-1 wiki iliyopita inatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na siku hiyo hiyo itafanya mazoezi Azam Complex.
    Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga, wote kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini Jumatano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS YAENDELEA KUJINOA KUIKABILI ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top