• HABARI MPYA

  Tuesday, February 25, 2014

  KIINGILIO CHA CHINI KABISA YANGA NA AL AHLY SH 7,000

  Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
  KIINGILIO cha chini katika mechi ya kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baina ya wenyeji Yanga SC na Al Ahly (National) ya Misri kitakuwa ni Sh. 7,000.
  Kiingilio hicho kitahusu watu watakaoketi jukwaa la viti vya rangi ya Chungwa, wakati VIP A tiketi moja itauzwa kwa Sh. 35,000 na kwa viti vya VIP B na C Sh. 25,000.
  Al Ahly watawasili Alfajiri ya kesho Dar es Salaam
  Al Ahly wanatarajiwa kuwasili Alfajiri ya kesho Dar es Salaam na kufikia katika hoteli ya Hyatt Regency, Kempinsky au Kilimanjaro Hotel, iliyopo maeneo ya Kivukoni.
  Waarabu hao wanaweza kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana, uliopo kando ya bahari ya Hindi na kikosi wanachotarajiwa kuja nacho Dar es Salaam ni makipa; Sherif Ekramy, Ahmed Adel Abdel-Monem na Mahmoud Abou El-Sooud.
  Mabeki ni; Wael Gomaa, Sherif Abdel-Fadil, Ahmed Fathi, Mohamed Naguib, Saad El-Din Samir, Sayed Moawad na Ahmed Shedid Qenawy.
  Viungo ni; Hossam Ashour, Shehab El-Den Ahmed, Ahmed Nabil Manga, Ahmed Shokry, Mahmoud ‘Trezeguet’, Rami Rabia, Walid Soliman, Abdullah El-Said na Mohamed Abou-Treika na washambuliaji El-Sayed Hamdy, Dominique  Da Silva, Emad Meteb na Amr Gamal ambaye ndiye tegemeo la mabao la timu hiyo kwa sasa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI KABISA YANGA NA AL AHLY SH 7,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top