• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 23, 2014

  TFF YAWAPA RAHA YANGA, WAFUTA GEMU NA PRISONS JUMATANO KUWAPA FURSA YA KUJIANDAA VYEMA NA WAARABU

  Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
  MECHI namba 118 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe Februari 26 mwaka huu itapangiwa tarehe nyingine.
  Uamuzi wa kuiondoa mechi hiyo iliyokuwa ichezwe Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umefanywa ili kuipa fursa zaidi Yanga kujiandaa kwa mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly ya Misri itakayofanyika Jumamosi (Machi 1 mwaka huu).

  Al Ahly na Yanga zitarudiana wiki moja baadaye kati ya Machi 7, 8 au 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAWAPA RAHA YANGA, WAFUTA GEMU NA PRISONS JUMATANO KUWAPA FURSA YA KUJIANDAA VYEMA NA WAARABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top