• HABARI MPYA

    Tuesday, February 18, 2014

    ZANZIBAR WAIKUMBUSHA YANGA AHADI YA KUWEKA KAMBI YA MICHUANO YA AFRIKA, WAWAAMBIA “AHADI NI DENI”

    Na Salum Vuai, Zanzibar
    KATIBU wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Khamis Abdalla Said ameikumbusha Yanga kuwa ‘ahadi ni deni’ na kwamba mashabiki wa soka Zanzibar wanasubiri kwa hamu kuwaona baada ya kuwakosa kwenye michuano ya Mapinduzi.
    Amesema ni vyema Yanga wawe waungwana kwa kutimiza ahadi waliyoitoa mbele ya Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi.
    Mnasubiriwa Zanzibar; Yanga SC imetakiwa kutimiza ahadi kwa kwenda kuweka kambi Zanzibar

    Aidha kwa kuwa waliahidi kupiga kambi hiyo kwa ajili ya mechi zao za Afrika na kutaka wapangiwe mechi kadhaa na (Chama cha Soka Zanziabr) ZFA ili fedha zitakazopatikana ziingie katika mfuko wa mashindano na wao hawatachukua hata shilingi.
    Kwa kuwa kamati inayo kumbukumbu ya ahadi hiyo na bado inakabiliwa na madeni yaliyotokana na gharama za kuziweka na kuzihudumia timu, inahitaji sana Yanga ije na kucheza ili kupata fedha hizo.
    Msemaji wa kamati Farouk Karim amesema amesoma pahala kwamba Yanga wanajiandaa kuweka kambi Bagamoyo au Chamazi, lakini anakusudia kuwasiliana na Makamu nMwenyekiiti wa klabu hiyo, Clement Sanga ili kumkumbusha ahadi yao na kuona vipi wataweza kuitekeleza.
    Lakini alisema kimsingi, Yanga inapaswa kuwa mkweli na kutimiza ahadi hiyo baada ya kujitoa kwenye mashindano ya Mapinduzi hatua iliyowakera mashabiki wa soka na Wazanzibari wote kwa jumla.
    Yanga SC imetinga Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuitoa Komorozine kwa jumla ya mabao 12-2, ikishinda 7-0 Dar es Salaam na 5-2 ugenini Moroni, Comoro.
    Sasa, mabingwa hao wa Bara watamenyana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam Machi 1 na marudiano kati ya Machi 7 na 9 mjini Cairo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR WAIKUMBUSHA YANGA AHADI YA KUWEKA KAMBI YA MICHUANO YA AFRIKA, WAWAAMBIA “AHADI NI DENI” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top