Na Mahmoud Zubeiry, Mombasa
WAKATI waliokuwa mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes tayari wapo nyumbani Kampala, Uganda tangu saa 7:00 mchana, kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kinaondoka saa 12:00 jioni kwa ndege kwenda Nairobi kujiandaa na mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya wenyeji, Kenya.
Stars iliwatoa mabingwa watetezi, Uganda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 katika Robo Fainali Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa, Kenya.
Uganda sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye Fainali za CHAN mwakani Afrika Kusini, baada ya kuvuliwa ubingwa wa Challenge.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Wish Yabarow wa Somalia, aliyesaidiwa na Kinde Mussa wa Ethiopia na Mohamed Idam wa Sudan, hadi mapumziko Stars ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1.
Mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Dani Sserunkuma alitangulia kuifungia Cranes bao dakika ya 16, baada ya kupokea krosi ya Hamisi Kiiza aliyemtoka Erasto Nyoni na kufumua shuti la chini lililompita kipa Ivo Mapunda.
Dakika mbili baadaye, Mrisho Ngassa aliisawazishia Stars baada ya kuwazidi ujanja na maarifa ya kisoka mabeki wa Uganda, akimalizia mpira uliopigwa na Mbwana Ally Samatta.
Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe ya DRC, aliangushwa chini nje kidogo ya eneo la hatari na mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akaenda kupiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja kuipatia Stars bao la pili.
Baada ya bao hilo, Stars waliendelea kuishambulia Uganda kwa kujiamini zaidi, lakini mabeki wa Cranes walisimama imara kutoruhusu mabao zaidi.
Kipindi cha pili, Stars ilipata pigo dakika ya 53 baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutolewa nje kwa nyekundu kwa kumchezea rafu Sserunkuma.
Uganda ikapata bao la kusawazisha dakika ya 73 kupitia kwa Martin Mpuga, aliyeunganisha kona ya Godfrey Walusimbi.
Kipa Ivo Mapunda alikuwa shujaa baada ya kuokoa penalti mbili za Dani Sserunkuma na Khalid Aucho wa Uganda na kuipa Stars ushindi wa penalti 3-2 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika hizo 90.
Mbali na kuokoa penalti hizo mbili, Uganda walipoteza penalti nyingine moja baada ya Godfrey Walusimbi kupiga, wakati Hamisi Kiiza Emannuel Okwi ndiyo pekee walioifungia Cranes penalti.
Waliofunga penalti za Bara ni Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’na Erasto Nyoni, wakati Mbwana Samatta na Amri Kiemba walikosa.
Hata hivyo, Stars ambayo itamkosa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi na Uganda jana, katika mchezo huo, pia iko hatarini kuwakosa wachezaji wake wawili tegemeo, Mrisho Khalfan Ngassa na Thomas Emmanuel Ulimwengu ambao ni majeruhi.
Ngassa aliumia na kutoka uwanjani dakika ya 80 jana akiwa tayari amefunga mabao mawili na kumpisha Athumani Iddi ‘Chuji’, wakati Ulimwengu alimaliza dakika 90 akiwa anachechemea kwa maumivu ya nyama.

![]() |
| Kikosi cha Stars kilichoivua ubingwa Uganda jana |

.png)
0 comments:
Post a Comment