• HABARI MPYA

    Sunday, July 07, 2013

    KIJANA AMFUNIKA MESSI KWA KUFUNGA BONGE LA BAO LA TIK TAK MAREKANI

    IMEWEKWA JULAI 7, 2013 SAA 8:37 MCHANA
    SI kama Lionel Messi amefunikwa, lakini hiki ndicho kilichotokea kwa nyota huyo wa Barcelona.
    Mchezaji wa Ridhaa, anayefanya kazi za utumishi wa fedha, alifanya vitu adimu katika mechi ya Hisani huko Chicago baada ya kufunga bao zuri la tik-tak.
    Matt Eliason alifanya kazi nzuri akichezea mechi ya Messi & Rafiki zake walioshinda 9-6 wachezaji wengine duniani, waliokuwa chini ya Nahodha, gwiji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry.
    Nenda chini kaangalie video
    Chest control: Matt Eliason tees up Thierry Henry's pass...
    Mpira kifuani: Matt Eliason akipokea kwa kifua pasi ya Thierry Henry...
    Head over heels: Eliason connects with his stunning overhead kick...
    Anapinduka: Eliason akifunga kwa tik tak...
    Net buster: The goalkeeper has no chance as Eliason scores his wonder goal
    Kitu nyavuni: Kipa hakuweza kuokoa mchomo hatari wa Eliason
    Eliason, alionekana bado hayuko tayari kuhimiliki vishindo vya MLS, alipokea pasi ya mpira wa adhabu uliopigwa na Henry akautuliza vizuri gambani na kupinduka tik tak dakika ya 28 ya mechi hiyo ya hisani. 
    "Wakati mpira ulipokuwa hewani, nilifikiria naweza kuupata mbele ya hao mashabiki wote,’ alisema Eliason.
    "Siyo kila siku unapata nafasi ya kucheza Messi. Hivyo nikafikiri lazima nijitume kujaribu bahati yangu, na bahati nzuri ikafanikiwa. 
    Messi and friends: Thierry Henry, Julio Cesar and Florent Malouda were among the big names playing at Soldier Field for the Barcelona superstar's charity match
    Messi na rafiki zake: Thierry Henry, Julio Cesar na Florent Malouda walikuwa miongoni mwa majina makubwa waliocheza kwenye Uwanja wa Soldier Field katika mechi ya hisani ya nyota huyo wa Barcelona
    Taking aim: Messi pleases the fans as he finds range with a long distance shot
    All smiles: Messi enjoys the game in front of a huge crowd in Chicago
    Messi akiwatuliza mashabiki wakati akienda kupiga shuti la mbali
    "Ni jambo la ajabu kucheza Uwanja naye.’
    Eliason, mchezaji wa zamani wa Chuo wa Northwestern Wildcats, alishangilia na mchezaji wa zamani wa Chelsea, kiungo Florent Malouda, kiungo wa Barcelona, Alex Song na baadaye akafurahi kwa kukumbatiana na Henry. 
    Bao lake ambalo limezagaa kwenye intaneti, linatarajiwa kumpa ulaji wa kuchezea klabu za soka ya kulipwa. 
    Na katika wakati huu wa dirisha la usajili zikiwa zimebaki wiki nane kabla halijafungwa, tunaweza kumuona Eliason akitua Ligi Kuu England msimu ujao? 
    Fan-tastic: American fans show their love for the Argentina ace with banners in support
    Babu kubwa: Mashabiki wa Marekani wakionyesha upendo wao kwa nyota wa Argentina kwa kubeba mabango ya kumuunga mkono
    Hands on: Julio Cesar shares a joke with Messi as former Fulham defender Carlos Bocanegra stands on
    Mikono: Julio Cesar akitaniana na Messi huku beki wa zamani wa Fulham, Carlos Bocanegra akiwa pembeni yao

    VIDEO: Angalia bao zuri lililofungwa mbele ya Messi...


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KIJANA AMFUNIKA MESSI KWA KUFUNGA BONGE LA BAO LA TIK TAK MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top