• HABARI MPYA

    Sunday, July 07, 2013

    AZAM VETERANS WATWAA UBINGWA MASHINDANO YA MWEZI MTUKUFU

    Mabingwa; Azam Veterans wakisherehekea baada ya ushindi
    Na Prince Akbar, IMEWEKWA JULAI 7, 2013 SAA 12:00 JIONI
    AZAM Veterans imechukua ubingwa wa michuano ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, baada ya kuifunga Vingunguti Veterans jioni hii kwenye Uwanja wa Tabata Shule, Dar es Salaam.
    Shujaa wa Azam jioni ya leo alikuwa Abdulkarim Amin ‘Popat’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 40 ya mchezo huo, akiunganisha pasi nzuri ya Hamisi Kikwa. 
    Kwa ushindi huo, Azam Veterans imezawadiwa seti mbili za jezi na mwandaaji wa mashindano hayo, Spear Mbwembwe, kipa wa zamani wa Simba SC na Lipuli ya Iringa. 
    Nahodha wa Azam Veterans, Abdulkarim Amin 'Popat' akipokea zawadi baada ya mechi


    Mfungaji Bora; Jemadari Said akipokea zawadi ya kiatu kwa kuwa mfungaji bora

    Mchezaji Bora; Nassor Idrisa akipokea zawadi ya Mchezaji Bora wa mashindano

    Aidha, mchezaji wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari ameibuka mfungaji bora wa mashindano hayo kwa mabao yake sita aliyofunga na Nassor Idrisa Mohammed ‘Father’ amekuwa mchezaji bora wa mashindano kutokana na kuongoza kutoa pasi za mabao pamoja na kuonyesha soka adimu. 
    Azam iliingia fainali baada ya kuifunga Kigamboni Veterans mabao 4-0 katika Nusu Fainali mchana wa leo, Jemadari peke yake akifunga matatu na lingine Abdallah Mohamed. 
    Awali ya hapo, Azam waliifunga TCC 6-1 na 3-1 katika hatua ya awali ya michuano hiyo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM VETERANS WATWAA UBINGWA MASHINDANO YA MWEZI MTUKUFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top