KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kushuka dimbani Jumamosi kumenyana na Bandari ya Kenya katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Azam FC inaendelea na mazoezi ya mwisho mwisho kuelekea michuano ya Ngao ya Jamii Jijini Tanga wiki ijayo baada ya kurejea Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kutoka Tunisia ambako iliweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya.
0 comments:
Post a Comment