• HABARI MPYA

  Sunday, March 12, 2023

  COASTAL UNION YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA SINGIDA STARS


  WENYEJI, Coastal Union wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Coastal Union walitangulia kwa bao la Greyson Gerlad dakika ya 44, kabla ya Singida Big Stars kusawazisha kupitia kwa Bright Adjei dakika ya 74.
  Kwa matokeo hayo, Coastal Union inafikisha pointi 26, ingawa inabaki nafasi ya 12, wakati Singida Big Stars inafikisha pointi 48 na kusogea nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA SINGIDA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top