• HABARI MPYA

  Sunday, March 12, 2023

  SENEGAL BINGWA NA AFCON U20 BAADA YA KUBEBA CHAN FEBRUARI


  TIMU ya taifa ya Senegal, 'Simba Wadogo wa Teranga' wamefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Vijana kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Gambia jana Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Jijini Cairo nchini Misri.
  'Simba hao Wadogo wa Teranga' jana wamecheza Fainali ya nne ya AFCON U20 baada ya kushika nafasi ya pili katika Fainali za 2015, 2017 and 2019.
  Na hili ni taji la pili kwa la Afrika ndani ya miezi miwili baada ya mapema Februari kutwaa Kombe la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kwa ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 na wenyeji, Algeria Uwanja wa Nelson Mandela Jijini Algiers.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SENEGAL BINGWA NA AFCON U20 BAADA YA KUBEBA CHAN FEBRUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top