• HABARI MPYA

  Sunday, March 12, 2023

  CHELSEA YAITANDIKA LEICESTER CITY 3-1 KING POWER


  TIMU ya Chelsea imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa King Power Jijini Leicester, Leicestershire.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Ben Chilwell dakika ya 11, Kai Havertz dakika ya 45 na ushei na Mateo Kovacic dakika ya 78, wakati la Leicester City limefungwa Patson Daka dakika ya 39.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 37 nafasi ya 10, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 24 nafasi ya 16 baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAITANDIKA LEICESTER CITY 3-1 KING POWER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top