• HABARI MPYA

  Sunday, March 12, 2023

  SALAH AKOSA PENALTI LIVERPOOL YACHAPWA 1-0


  BAO pekee la Philip Billing dakika ya jana liliwapa wenyeji, AFC Bournemouth ushindi wa 1-0 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vitality, Bournemouth, Dorset.
  Ushindi huo unaifanya AFC Bournemouth ifikishe pointi 24 na kusogea nafasi ya 17, wakati Liverpool inabaki na pointi zake 42 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 26.
  Katika mchezo huo, mshambuliaji Mohamed Salah alikosa penalti dakika ya 69 ambayo ilitolewa kwa msaada wa VAR baada ya mpira wa kichwa wa Diogo Jota kumgonga mkononi Adam Smith.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AKOSA PENALTI LIVERPOOL YACHAPWA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top