• HABARI MPYA

  Sunday, January 09, 2022

  MCHENGERWA WAZIRI MPYA WA MICHEZO, NAIBU YULE YULE


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amemteua Mohamed Omary Mchengerwa kuwa Waziri mpya wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.
  Mchengerwa akichukua nafasi ya mwana Yanga mwenzake, Innocent Innocent Lugha Bashungwa aliyehamishiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  Naibu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo anaendelea kuwa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Philipo Gekul.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHENGERWA WAZIRI MPYA WA MICHEZO, NAIBU YULE YULE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top