• HABARI MPYA

  Wednesday, January 05, 2022

  CHILUNDA AING’ARISHA AZAM FC KOMBE LA MAPINDUZI


  BAO pekee la mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda limeipa mwanzo mzuri Azam FC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Meli 5 City katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jumanne Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mechi iliyotangulia jioni, timu nyingine ya Bara, Namungo ilishinda pia 2-0 dhidi ya wenyeji wengine, Yosso Boys, Kundi A pia hapo hapo Uwanja wa Amaan.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 53 na Relliant Lusajo dakika ya 90 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita kufuatia kuilaza Meli 4 City katika mchezo wa kwanza Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHILUNDA AING’ARISHA AZAM FC KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top