• HABARI MPYA

  Friday, January 07, 2022

  AZAM FC YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 KOMBE LA MAPINDUZI


  BAO pekee la kiungo Mkenya, Kenneth Muguna dakika ya 67 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mechi iliyotangulia, ya Kundi A pia, Meli 4 City imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Yosso Boys hapo hapo Uwanja wa Amaan, mabao ya Hussein Mwinyi dakika ya 18, Said Omar dakika ya 45' na Ali Mmanga dakika ya 81.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top