• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 03, 2020

  SEMINA NA MAFUNZO MAKUBWA YA KARATE KUFANYIKA SONGEA IJUMAA HADI JUMAPILI WIKI HII

  Na Mwandisji Wetu, SONGEA
  SEMINA na mafunzo makubwa ya mchezo wa Karate nchini (GASSHUKU 2020) vitafanyika mkoani kuanzia Ijumaa hadi Jumapili wiki hii Songea mkoani Ruvuma.
  Wacheza Karate ambao tayari wamewasili Ruvuma wameahidi kufanyia kazi mafunzo hayo, lengo likiwa ni kuutangaza mchezo huo na kuangalia viwango vya wachezaji wote Tanzania.
  Semina na mafunzo hayo vinaandaliwa na Shirikisho la Mchezo wa Karate Tanzania (JKA/WF-TZ) na vitaongozwa na Mkufunzi mkuu wa Karate nchini, Sensei Jerome Mhagama na msaidizi wake, Mikidadi Kilindo.


  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Solomon Mndeme ndiye anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Semina na mafunzo hayo.
  Zoezi hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa tofauti na mwaka jana wenueji walikuwa mkoa wa Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SEMINA NA MAFUNZO MAKUBWA YA KARATE KUFANYIKA SONGEA IJUMAA HADI JUMAPILI WIKI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top