• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 06, 2020

  KOEMAN HALI TETE BARCELONA, YACHAPWA 2-1 NA CADIZ LA LIGA


  TIMU ya Barcelona jana imechapwa 2-1 na wenyeji, Cadiz katika mchezo wa  La Liga Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan. Mabao ya Cadiz yalifungwa na Alvaro Gimenez dakika ya nane na Alvaro Negredo dakika ya 63, wakati la Barcelona Alcala alijifunga dakika ya 57.
  Kwa matokeo hayo, Cadiz wanafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 12 na kupanda nafasi ya tano, wakizidiwa pointi mbili na Real Madrid na Villarreal zinazofuatana nafasi ya tatu na ya nne zikiwa zimecheza mechi 11.
  Kikosi cha Ronald Koeman, Barcelona kinabaki na pointi zake 14 baada ya kucheza mechi 14 katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa La Liga 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOEMAN HALI TETE BARCELONA, YACHAPWA 2-1 NA CADIZ LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top