• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 06, 2020

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA MWADUI FC 1-0 MOROGORO, IHEFU YATOA SARE YA 1-1 NA JKT TANZANIA MBEYA

  BAO la dakika ya saba la mshambuliaji Riffat Msuya limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi 14 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati Mwadui inabaki na pointi zake 10 za mechi 14 katika nafasi ya 17 kwenye ligi ya 18, ambayo mwisho mwa msimu timu nne zitateremka daraja.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Ihefu SC imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT Tanzania Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Joseph Kinyozi alianza kuifungia Ihefu SC dakika ya 46, kabla ya Hassan Twalib kuisawazishia JKT Tanzania dakika ya 90 na ushei.


  Sasa Ihefu imefikisha pointi saba baada ya kucheza mechi 14, ingawa inaendelea kusbhika, wakati  JKT Tanzania imefikisha pointi 11 kufuatia kucheza mechi 14 pia, japokuwa nayo inabaki nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA MWADUI FC 1-0 MOROGORO, IHEFU YATOA SARE YA 1-1 NA JKT TANZANIA MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top