• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 06, 2020

  CHELSEA YAWATANDIKA LEEDS UNITED 3-1NA KUPANDA KILELENI ENGLAND


  CHELSEA jana imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Mabao ya Chelsea yalifungwa na Olivier Giroud dakika ya 27, Kurt Zouma dakika ya 31 na Christian Pulisic dakika ya 90 na ushei baada ya Leeds United kutangulia kwa bao la Patrick Bamford dakika ya nne.
  Kwa ushindi huo, The Blues inafikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi 11 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikiwazidi pointi moja Tottenham Hotspur na Liverpool ambao wamecheza mechi 10   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAWATANDIKA LEEDS UNITED 3-1NA KUPANDA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top