• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 04, 2020

  ITABA ACHUKUA NAFASI YA DULLAH MBABE PAMBANO NA MKONGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BONDIA maarufu, Abdallah Pazy “Dulla Mbabe” ameondolewa kuzipiga na bondia kutoka DR Congo Alex Kabangu na nafasi yake imechukuliwa na Hussein Itaba.
  Pambano hilo limepangwa kufanyika Novemba 13 kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Oysterbay na ambapo siku hiyo pia bondia nyota nchini Hassan Mwakinyo atapigana na bondia Jose Carlos Paz kutoka Argentina akiwania mikanda miwili.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Jackson Sport, Kelvin Twissa alisema jana kuwa mabadiliko hayo ni kawaida kutokea katika masuala ya ngumi za kulipwa bondia huyo (Itaba) ameanza mazoezi kwa ajili ya kupambana na Kabangu.
  Hivi karibuni, Mbabe alipigwa kwa pointi dhidi ya bondia  Bek Nurmaganbet mjini Atyrau, Kazakhstan. Bondia huyo alikwenda kupigana chini ya promota Jay Msangi.

  “Tumeona tufanye mabadiliko katika moja ya pambano letu kwa lengo la kupanua wigo na kujenga heshima katika ngumi za kulipwa nchini, hivyo mabadiliko hayo yamefanywa ili kupanua wigo wa mabondia na kuinua vipaji zaidi hapa nchini, naamini Itaba atafanya vyema katika pambano hilo,” alisema Twissa.
  Alisema kuwa maandalizi ya mapambano ya ‘Dar Fight Night’ yanaendelea vizuri huku bondia bingwa wa mabara wa uzito wa superwelter Hassan Mwakinyo akijifua vikali.
  Mbali ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara  wa uzito huo huo wa Chama cha IBA.
  Mabondia kutoka nchi tano watazichapa kumsindikiza Mwakinyo na Paz, akiwamo aliyekuwa bingwa wa dunia wa WBC, Fatuma Zarika kutoka Kenya. Zarika atazichapa na Patience Mastara wa  Zimbabwe, na Zulfa Yusuph Macho atacheza na Alice Mbewe wa Zimbabwe.
  Alisema kuwa wameamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi kutokana na kutambua vipaji vya mabondia mbalimbali hasa Mwakinyo ambaye anafanya vizuri katika mapambano yake.
  "Siku hiyo kutakuwa na pambano  makubwa ambapo mabondia kutoka nchi sita, Argentina, DR Congo, Kenya, Zimbabwe na wenyeji Tanzania watapigana, ni siku ambayo mashabiki wa ngumi za kulipwa wataona kitu tofauti kabisa katika mchezo huo, " alisema Twisa.
  Alisema kuwa kampuni yao chini ya udhamini wa Azam TV, colosseum hotel Dar es salaam na Asas  ina uzoefu mkubwa katika kuandaa matamasha, masoko na shughuli mbalimbali na kuahidi kufanya jambo la kihistoria hapa nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ITABA ACHUKUA NAFASI YA DULLAH MBABE PAMBANO NA MKONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top