• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 04, 2020

  LEWANDOWSKI APIGA MBILI BAYERN MUNICH YASHINDA 6-2 UGENINI


  MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Bayern Munich 
  mabao mawili dakika ya 21 kwa penalti na 88 akimalizia pasi ya Javi Martínez katika ushindi wa 6-2 dhidi ya wenyeji, FC Salzburg kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena. Mabao mengine ya Bayern Munich yalifungwa na Rasmus Kristensen aliyejifunga dakika ya 44, Jerome Boateng dakika ya 79, Leroy Sane dakika ya 83 na Lucas Hernandez dakika ya 90 na ushei, wakati ya FC Salzburg yalifungwa na Mergim Berisha dakika ya nne na Masaya Okugawa dakika ya 66. Kwa ushindi huo, bayern Munich inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza kundi kwa ponti tano zaidi ya Atletico Madrid inayofuatia 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LEWANDOWSKI APIGA MBILI BAYERN MUNICH YASHINDA 6-2 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top