• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 05, 2020

  AZAM FC YAWATANDIKA DODOMA JIJI FC MABAO 3-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na Mromania, Aristica Cioaba inafikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 10, sasa ikiwazidi ponti mbili vigogo, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Katika mchezo huo, mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Aggrey Morris dakika ya 47, kiungo mshambuliaji Ayoub Lyanga dakika ya 58 na beki Hassan Kapona aliyejifunga akijaribu kuokoa krosi ya kiungo Mzimbabwe, Never Tigere dakika ya 62.

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Hamad Majimengi dakika ya 56 limetosha kuwapa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
  Mbeya City ikalazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya. Kibu Dennis alianza kuwafungia wenyeji dakika ya saba, kabla ya Hassan Nassor kuwasawazishia wageni dakika ya 45 na ushei. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWATANDIKA DODOMA JIJI FC MABAO 3-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top