• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 01, 2020

  SANCHO APIGA HAT TRICK NA KULAANI MAUWAJI YA GEORGE FLOYD

  Nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho alionyeshwa kadi ya njano kwa kuvua jezi kuonyesha fulana yenye maandishi 'Justice for George Floyd' akilaani tukio la kuuawa kwa Mmarekani mweusi, George Floyd aliyeuliwa kikatili na Polisi. Sancho alifanya hivyo katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya wenyeji, Paderborn jana Uwanja wa Benteler-Arena akifunga mabao matatu dakika za 57, 74 na 90 na ushei katika ushindi wa 6-1. Mabao mengine ya Borussia Dortmund yalifungwa na Thorgan Hazard dakika ya 54, Achraf Hakimi dakika ya 85 na Marcel Schmelzer dakika ya 89 wakati bao pekee la Paderborn lilifungwa na Uwe Hunemeier kwa penalti dakika ya 72 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SANCHO APIGA HAT TRICK NA KULAANI MAUWAJI YA GEORGE FLOYD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top