• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 22, 2018

  REAL MADRID KUBEBA KLABU BINGWA YA DUNIA BILA RONALDO

  KWA msimu wa tatu mfululizo klabu ya Real Madrid inafika fainali ya Klabu bingwa ya dunia, lakini safari hii wanaingia uwanjani bila Cristiano Ronaldo ambaye mwanzoni mwa msimu alijiunga na Klabu ya Juventus. Real Madrid wamefika fainali baada ya kuwafunga Kashima Antlers 3-1 siku ya Jumatano.
  Katika mchezo wa fainali Real Madrid watacheza dhidi ya Al Ain FC kutoka Falme za Kiarabu. Fainali za Klabu bingwa ya Dunia mwaka huu zinachezwa katika jiji la Al Ain, Abu Dhabi ambapo ndio nyumbani kwa klabu ya Al Ain FC. Al Ain FC wao wamefika fainali baada ya kuwafunga River Plate kwa mikwaju ya penati siku ya jumanne. 

  Kikosi cha sasa cha Real Madrid bila nyota wake, Cristiano Ronaldo (pichani chini)

  Mchezo wa fainali utapigwa leo jumamosi majira ya saa 1:30 Usiku saa za Afrika Mashariki na utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football kwenye king’amuzi cha StarTimes pekee.
  Pia kutakuwa na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ambao utapigwa mapema saa 10:30 jioni na kuwakutanisha Kashima Antlers dhidi ya River Plate. Mchezo huo pia utaonyeshwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee.
  Wateja wa StarTimes wataweza kuona mechi zote hizi pamoja na Bundesliga kwa kulipia kifurushi cha MAMBO Tsh 14,000 tu kwa watumiaji wa Antenna na kifurushi cha SMART Tsh 21,000 tu kwa watumiaji wa dikoda za Dish. StarTimes pekee ndio wenye kibali cha kuonyesha michuano hii nchini Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID KUBEBA KLABU BINGWA YA DUNIA BILA RONALDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top