• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 27, 2018

  LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA BARA KUANZA JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite inatarajia kuanza Jumamosi ya Desemba 29, 2018 ikishirikisha timu 12 kwa mfumo wa nyumbani na ugenini.
  Akizungumza kuelekea kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Serengeti Premium Lite, Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake Amina Karuma amesema msimu huu utakua na ushindani mkubwa.
  Amesema kwa namna timu zote zilivyojiandaa na kwa udhamini wa kinywaji cha Serengeti Lite,inaifanya ligi kuongeza ushindani zaidi.
  “Ni ukweli usiopingika kwamba ligi yetu ya wanawake ambayo inadhaminiwa na Serengeti Premium Lite inaongezeka chachu ya ushindani na tunatarajia msimu unaoanza utakua na ushindani zaidi” amesema Karuma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania(TWFA) Amina Karuma (kushoto) akipokea Fulana kutoka kwa Afisa Masoko na Udhamini wa SBL, George Mango kwa ajili ya timu za Ligi Kuu itakayoanza Jumamosi

  Kwa upande wake, Afisa masoko wa Serengeti Breweries Bw. George Mango amesema wamejiandaa vya kutosha kuwezesha mashindano hayo kuonesha msisimko ili kuwapatia burudani mashabiki wa mpira wa miguu pamoja na kutoa ushindani mkubwa wa soka la wanawake kupitia bia murua ya Serengeti Premium Lite.
  “Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium Lite imewekeza kiasi cha Shilingi milioni 450 ili kuwezesha ligi hii ya wanawake iwe ya ushindani mkubwa na kuwaletea msisimko mashabiki wa soka hapa nchini,” alisema George na kubainisha kwamba maandalizi ya kuwezesha michuano hiyo yamekamilika.
  “Watanzania wakae tayari sasa kuona burudani maridhawa kutoka kwa timu zinazoshiriki ligi hii. Hakika ni ligi inayotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu sana,” alisema. “Tumeona namna ambavyo ligi ilivyoweza kutoa misisimko na msimu huu timu zimeongezeka kutoka 8 kwenye ligi mwaka jana hadi 12 za sasa,”
  Bia ya Serengeti Lite ni kinywaji murua kinachozalishwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited. Mbali na bia hii, Serengeti Breweries pia hutengeneza na kusambaza vinywaji mbalimbali, ikiwemo bia ya Serengeti Premium Lager, iliyojizoelea tuzo kadhaa za kimataifa kwa ubora, inayodhamini timu ya taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars.  
  Timu 12 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Tanzania Bara ni Kigoma Sisterz ya Kigoma, JKT Queens, Simba Queens, Yanga Princess, Evergreen za Dar es Salaam, Alliance Girls, Marsh Academy za Mwanza, Baobab Queens ya Dodoma, Mlandizi Queens ya Pwani, Panama ya Iringa, Mapinduzi Queens ya Njombe na Tanzanite ya Arusha..
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA BARA KUANZA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top