• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 18, 2018

  MAN UNITED YAMFUKUZA MOURINHO, BLANC KUCHUKUA NAFASI

  KLABU ya Manchester United imemfukuza kocha wake, Mreno Jose Mourinho baada ya mwenendo mbaya wa timu katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya England.
  Mourinho anaondoka timu hiyo baada ya miaka miwili na nusu kufuatia mwanzo mbaya kabisa kwenye timu hiyo tangu mwaka 1990. 
  Na hiyo ni baada ya kipigo cha 3-1 kutoka kwa Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumapili Uwanja wa Anfield.
  Klabu hiyo imetoa taarifa leo asubuhi kwamba : "Manchester United inatangaza kwamba Jose Mourinho ameondoka kwenye timu mara moja,".

  Mreno Jose Mourinho amefukuzwa Manchester United baada ya mwanzo mbaya katika Ligi Kuu ya England  

  Na sasa baada ya kumfukuza kocha huyo mwenye umri wa miaka 65, klabu itateua kocha wa muda atakayeiongoza hadi mwishoni mwa msimu.
  Beki wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Laurent Blanc ndiye anatarajiwa kupewa nafasi hiyo katika klabu aliyoichezea kati ya mwaka 2001 na 2003.
  Blanc aliyechezea pia Barcelona ya Hispania na Inter Milan ya Italia, amewahi kufundisha timu za Bordeaux, Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAMFUKUZA MOURINHO, BLANC KUCHUKUA NAFASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top