• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 21, 2018

  KASEJA AIPELEKA KMC 32 BORA KOMBE LA TFF, RUVU YATUPWA NJE NA TIMU YA ‘MCHANGANI’

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imefanikiwa kwenda hatua ya 32 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya kufuatia sare ya 0-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa kipa mkongwe wa KMC, Juma Kaseja aliyeokoa penalti ya mwisho ya Tanzania Prisons iliyopigwa na Jeremiah Juma na kuivusha timu yake hatua ya 32 Bora ya ASFC. 
  Timu ya Mighty Elephant imeitupa nje Ruvu Shooting ya Pwani kwa mikwaju ya penalti pia 6-5, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

  Mechi nyingine za leo, La Familia imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mawenzi Market, Coastal Union ikaichapa Changanyikeni 4-1-4 Coastal Union na Alliance FC ya Mwanza ikaichapa Mufindi United 3-0.
  Maana yake, timu zilizofuzu kuingia raundi inayofuata ni KMC, La Familia, Coastal Union, Mighty Elephant na Alliance FC.
  Na hiyo inamaanisha Ruvu Shooting na Tanzania Prisons zinakuwa timu za kwanza kabisa za Ligi Kuu Tanzania ya Bara kutupwa nje ya michuano hiyo msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KASEJA AIPELEKA KMC 32 BORA KOMBE LA TFF, RUVU YATUPWA NJE NA TIMU YA ‘MCHANGANI’ Rating: 5 Reviewed By: Mwakasege Blog
  Scroll to Top