• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 19, 2018

  POGBA KUPIGWA FAINI KWA KUMKEJELI MOURNHO INSTAGRAM

  KIUNGO Paul Pogba anatarajiwa kupigwa faini na klabu yake, Manchester United kwa kuposti picha ya kumkejeli na kumvunjia heshima alihyekuwa kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho aliyefukuzwa.
  Pogba aliposti picha ya kumkebehi Mourinho katika ukurasa wake wa Instagram jana na kuweka ujumbe wa ‘Iandikie maelezo hii’.
  Posti hiyo aliifuta dakika 10 baadaye baada ya kupata likes zaidi ya 64,000 ambayo ilimvutia hadi mchambuzi wa Sky Sports, Gary Neville aliyeandika: ‘Unaweza kuandika moja nawe pia!’

  Posti hiyo iliwaudhi mabosi wa United ambao wanaamini ilikuwa mbaya na kumvunjia heshima mchezaji huyo ghali wa klabu aliyesajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 89. 
  Pogba, anayelipwa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki Old Trafford anatarajiwa kupigwa faini kwa kitendo chake.
  Inafahamika Mfaransa huyo alikuwa haelewani na Mourinho kiasi cha Pogba kuvuliwa Unahodha Msaidizi wa klabu Septemba na aliwekea benchi muda wote kwenye mechi mbili zilizopita za ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: POGBA KUPIGWA FAINI KWA KUMKEJELI MOURNHO INSTAGRAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top