• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 21, 2018

  MSHAMBULIAJI WA SIMBA SC AJIUNGA NA AFC LEOPARDS YA KENYA KWA MKOPO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI chipukizi Mtanzania, Marcel Boniventure Kaheza amejiunga na klabu ya AFC Leopards ya Kenya kwa mkopo kutoka Simba SC ya Dar es Salaam.
  Taarifa ya Simba SC kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba, Kaheza ni miongoni mwa wachezaji wanne iliyowatoa kwa mkopo kwenda klabu mbalimbali.
  Wengine ni kipa Said Mohammed Ndunda aliyepelekwa Ndanda FC ya Mtwara na washambauliaji Mohammed Rashid KMC ya Kinondoni na Salum Juma Ishaka, mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 anayekwenda Ashanti FC ya Ilala.

  Marcel Kaheza amejiunga na AFC Leopards ya Kenya kwa mkopo kutoka Simba SC 

  Wakati hao wakitoka, Simba SC imesajili mchezaji mmoja tu katika dirisha dogo ambaye ni Zane ‘Cafu' Coulibaly raia wa Burkina Faso aliyekuwa anachezea klabu ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast.
  Beki huyo wa kulia amesajiliwa kuziba pengo la beki mzawa, Shomari Kapombe aliyeumia mwezi uliopita akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars ambaye atakuwa nje kwa muda mrefu.
  Coulibaly alianza kuitumikia Simba SC Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI WA SIMBA SC AJIUNGA NA AFC LEOPARDS YA KENYA KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top