• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 19, 2018

  OLE GUNNAR SOLSKJAER APEWA UKOCHA WA MUDA MANCHESTER UNITED

  KLABU ya Manchester United imemtambulisha mchezaji wake wa zamani, Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wake wa muda.
  Jana usiku, kiasi cha saa 12 baada ya kufukuzwa kwa Jose Mourinho, tovuti ya United iliposti video yenye maelezo: 'Solskjaer anakuwa kocha wetu wa muda, misimu 20 tangu tuchukue mataji matatu kwa bao hili Camp Nou...’.
  Video hiyo ambayo inakumbushia bao la ushindi la mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1999, haikutokea kwenye ukurasa wa mwanzo wa tovuti hiyo ya klabu bali ilipostiwa URL yake. 

  Manchester United inatarajiwa kumtambulisha Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wake wa muda kuchukua nafasi ya Jose Mourinho

  MECHI ZA KWANZA ZA SOLSKJAER MAN UTD 

  Ligi Kuu ya England
  Saturday Cardiff City (ugenini)
  Boxing Day Huddersfield Town (nyumbani)
  Decemba 30 Bournemouth (nyumbani)
  Januari 2 Newcastle United (ugenini)
  Januari 5 Reading (nyumbani)
  Kombe la FA Raundiya Tatu
  Januari 13 Tottenham (ugenini) 
  Baadaye United waliondoa habari hiyo kabla ya kuipandisha tena baada ya kumtambulisha rasmi kocha huyo wa Molde kuwa mrithi wa Mourinho kumalizia msimu.
  Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg mara moja aliandika ujumbe wa kumpongeza Solskjaer usiku wa jana katika tweet ambayo baadaye aliifuta. 
  Solskjaer, aliyefunga zaidi ya mabao 100 katika miaka yake 11 ya kuichezea klabu ya Old Trafford, atasaidiwa na aliyekuwa Msaidizi namba mbili wa Sir Alex Ferguson, Mike Phelan kumalizia msimu.
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 amesema kwamba atakapomaliza majukumu yake atarejea Molde, ambao msimu wao wa ligi unaanza mwishoni mwa mwezi Machi.
  Lakini inafahamika kwamba kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino anabaki kuwa mtu anayetakiwa kwa muda mrefu na United na vyanzo vimekwishaweka wazi juu ya dhamira yake kufanya kazi Old Trafford. 
  Muargentina huyo alikuwa chaguo la Sir Ferguson kabla ya Mourinho kuajiriwa mwaka 2016 na inafahamika United imekiwshafanya jaribio la kumng’oa Spurs, lakini watakutana na kikwazo kutoka kwa mkuu wa Tottenham, Daniel Levy, aliyemsainisha mkataba wa miaka mitano mwezi Mei.
  Hakuna namna ya kukwepa kumnunua na maana yake Man United watalazimika kulipa Pauni Milioni 40 kumpata mtu wamtakaye.
  Watakutana pia upinzani kutoka kwa Real Madrid ambao walikuwa tayari kumpa ofa kocha huyo wa zamani wa Espanyol mwenye umri wa miaka 46 ahamie Bernabeu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: OLE GUNNAR SOLSKJAER APEWA UKOCHA WA MUDA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top