• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 22, 2018

  MTIBWA SUGAR WAPIGWA NJE, NDANI NA KUTOLEWA KIZEMBE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kwa vipigo vya nyumbani na ugenini baada ya leo kuchapwa 2-1 na KCCA ya Uganda Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Kwa kipigo hicho, Mtibwa Sugar inatupwa nje kwa jumla ya mabao 5-1, baada uya kuchapwa 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda.
  Katika mchezo wa leo, iliwachukua dakika 26 tu KCCA kupata bao lao la kwanza kupitia kwa Muzamiru Mutyaba aliyepiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya Steven Sserwadda.

  Salum Kihimbwa ameifungia bao pekee Mtibwa Sugar leo ikichapwa 2-1 na KCCA Chamazi

  Mtibwa Sugar wakasawazisha bao hilo dakika ya 51 kupitia kwa kiungo Salum Kihimbwa aliyeunganisha kona nzuri ya beki wa kulia, Salum Kanoni.
  KCCA wakawazima wenyeji kwa bao la dakika ya 86 la nyota wake, Allan Okello aliyewapita kwa urahisi mabeki wa Mtibwa Sugar waliokuwa wamezubaa.
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Shaaban Kado, Salum Kanoni, Dickson Daudi/Hassan Isihaka dk62, Shaaban Nditi, Ismail Mhesa/Haruna Chanongo dk53, Cassian Ponera, Saleh Abdallah, Salum Kihimbwa, Juma Luizio/Riphat Msuya dk57, Jaffar Kibaya na Issa Issa.
  KCCA: Charles Lukwago, Lawrence Bukenya, Awany Timothy, Jackson Nunda/Gift Abubakar dk56, Muzamiru Mutyaba, Allan Kyambadde/ Herbert Achai dk78, Mustafa Kizza, Eric Ssenjobe, Steven Sserwadda, Charles Lukwago, Allan Okello na Filbert Obenchan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAPIGWA NJE, NDANI NA KUTOLEWA KIZEMBE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top