• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 19, 2018

  KOCHA WA ZAMANI WA YANGA APEWA TIMU YA TAIFA ESWATINI

  SHIRIKISHO la Soka Eswatini limemthibitisha kocha wa zamani wa Yanga SC ya Tanzania na Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Mserbia, Kosta Papic kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  Papic anachukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha Mholanzi, Peter De Jongh kufundisha timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo zamani ilikuwa inajulikana kama Swaziland.
  Na maana yake aliyekuwa kocha wa muda wa timu hiyo, Anthony Mdluli ameachia ngazi rasmi leo.
  Rais wa EFA, Adam Mthethwa amesema kwamba mabadiliko hayo ni mkakati wa kuinua tena soka ya nchi hiyo kuanzia mwakani chini ya Mserbia huyo.

  Papic anatarajiwa kuwasili nchini humo wiki ya kwanza ya Januari kuanza majukumu yake. 
  Mtihani wake wa kwanza utakuwa ni mechi dhidi ya Sihlangu na Tunisia kufuzu Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019, utakaofuatiwa na michuano ya COSAFA Challenge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA WA ZAMANI WA YANGA APEWA TIMU YA TAIFA ESWATINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top