• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 16, 2018

  MBWANA SAMATTA AIFUNGIA BAO LA PILI KRC GENK YAIBUKA NA USHINDI WA 2-0 KATIKA LIGI YA UBELGIJI LEO

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa leo ameifungia bao la pili timu yake, KRC Genk ikishinda 2-0 dhidi ya KV Oostende kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alifunga bao hilo dakika ya 74 akimalizia pasi ya kiungo hodari Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero, baada ya kiuno wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 33. 
  Ushindo huo unaifanya KRC Genk ijiongezee pointi tatu na kufikisha pointi 42 baada ya kucheza mkechi 19, sasa ikiwazidi kwa pointi saba, Club Brugge inayoshika nafasi ya pili.
  Mbwana Samatta akiruka kushangilia baada ya kuifungia KRC Genk bao la pili leo 
  Mbwana Samatta akimtoka mchezaji wa KV Oostende leo Uwanja wa Luminus Arena 
  Mbwana Samatta akibinuka tiktak katikati ya wachezaji wa KV Oostende leo 
  Mbwana Samatta akimvaa kipa KV Oostende, Mcameroon Fabrice Ondoa leo mjini Genk

  Samatta leo amecheza mechi ya 134 katika mashindano yote tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa jumla ya mabao 53.
  Katika Ligi ya Ubelgiji pekee amefikisha mechi 104 na kufunga mabao 38, Kombe la Ubelgiji mechi nane na mabao mawili na Europa League mechi 22 mabao 14.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest, Uronen, Heynen, Malinovskyi/Berge dk55, Pozuelo/Seck dk75, Ndongala/Paintsil dk84, Trossard na Samatta.
  KV Oostende; Ondoa, Faes, Milovic, Lombaerts, Guri/Boonen dk71, Nkaka, Bataille, Vandendriessche, Capon/Zivkovic dk69, Coopman na Canesin/Marquet dk80.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBWANA SAMATTA AIFUNGIA BAO LA PILI KRC GENK YAIBUKA NA USHINDI WA 2-0 KATIKA LIGI YA UBELGIJI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top