• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 17, 2018

  MESSI APIGA HAT TRICK YA 31 LA LIGA BARCELONA IKISHINDA 5-0

  Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona mabao matatu dakika za 43, 47, na 60 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya wenyeji, Levante usiku wa jana Uwanja wa Ciudad de Valencia, hiyo ikiwa hat trick yake ya 31 katika La Liga. Mabao mengine ya Barca yamefungwa na Luis Suarez dakika ya 35 na Gerard Pique dakika ya 88 na sasa timu hiyo inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 16, sasa ikizizidi kwa pointi tatu Sevilla na Atletico Madrid zinazofuatia kwenye nafasi ya pili na ya tatu 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI APIGA HAT TRICK YA 31 LA LIGA BARCELONA IKISHINDA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top