• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 17, 2018

  SERENGETI BOYS YAREJEA LEO BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA KANDA TANO AFRIKA KWA KUIPIGA ANGOLA JANA BOTSWANA

  Na Mwandishi Wetu, GABORONE
  KIKOSI cha Tanzania kinarejea leo Dar es Salaam baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa soka wa vijana chini ya umri wa miaka 17 Kusini mwa Afrika (Kanda ya Tano) jana mjini Gaborone nchini Botswana.
  Serengeti Boys imetwaa ubingwa wa wa U17 Kanda ya Tano Afrika baada ya ushindi wa penalti 6-5 dhidi ya Angola kufuatia sare ya bao 1-1, kwenye mchezo wa fainali jana mjini Gaborone nchini Botswana.
  Katika dakika 120 za mchezo huo, Angola walitangulia kwa bao la Morais kabla ya Tanzania kusawazisha kupitia kwa Kelvin Pius dakika ya 78.
  Wachezaji wa Tanzania wakifurahia na taji lao na michuano ya Kanda ya Tano Afrika 

  Nahodha wa Tanzania, Michael Morice akikabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi ya fainali jana

  Na baada ya mchezo huo, Nahodha wa Tanzania, Michael Morice alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi.
  Tanzania iliyo chini ya kocha Oscar Milambo ilifika hatua hii kwa ushindi wa matuta pia, ikiitoa Zambia kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 pia. 
  Awali, katika mechi za Kundi B, Serengeti Boys ilizifunga Malawi 2-1 na Afrika Kusini 2-0 baada ya kufungwa 2-0 na Angola, hivyo kufanikiwa kuingia Nusu Fainali.
  Kikosi cha Serengeti Boys kinachojiandaa kwa fainali za Afrika za U17 Mei mwakani ambazo watakuwa wenyeji katika Jiji la Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAREJEA LEO BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA KANDA TANO AFRIKA KWA KUIPIGA ANGOLA JANA BOTSWANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top