• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 22, 2018

  MAN CITY WANOGEWA NA VIPIGO, WACHAPWA TENA 3-2 NYUMBANI

  Gabriel Jesus wa Manchester City (kulia) akiudhibiti mpira dhidi ya James Tomkins wa Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad.
  Crystal Palace imeshinda 3-2, mabao yake yakifungwa na Jeffrey Schlupp dakika ya 33, Andros Townsend dakika ya 35 na Luka Milivojevic kwa penalti dakika ya 51, wakati ya Man City inayopoteza mechi ya pili ya msimu yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya 27 na Kevin De Bruyne dakika ya 85.
  Crystal Palace inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 18 na kujivuta hadi nafasi ya 14 kutoka ya 16, wakati Man City inabaki na pointi zake 44 za mechi 18 katika nafasi ya pili, nyuma ya Liverpool yenye pointi 48 za mechi 18 pia 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY WANOGEWA NA VIPIGO, WACHAPWA TENA 3-2 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top