• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 24, 2018

  SAMATTA APIGA ZOTE MBILI KRC GENK YASHINDA 2-0 UGENINI LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, EUPEN
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumapili amefunga mabao yote mawili, timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 2-0 katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji dhidi ya AS Eupen Uwanja wa Kehrweg mjini Eupen.
  Samatta aliyekuwa anasherehekea kufikisha umri wa miaka 26 tangu azaliwe, alifunga mabao yake katika dakika za 13 na 20 akimalizia pasi ya beki Mfinland, Jere Uronen
  Kwa ushindi huo, Genk inafikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 20, ikiendelea kuongoza Jupiter Ligue kwa pointi  saba zaidi ya Club Brugge iliyopo nafasi ya pili.
  Samatta amefikisha mechi 136 za kuichezea KRC Genk katika mashindano yote akiwa amefunga jumla ya mabao 53.

  Mbwana Samatta akifurahia baada ya kuifungia KRC Genj mabao mawili Jumapili
  Mbwana Samatta akimpita kipa wa AS Eupen, Hendrik Van Crombrugge
  Kwenye Europa League amecheza mechi 22 na kufunga mabao 14, Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 104 na kufunga mabao 38 na katika Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa.
  Kikosi cha KAS Eupen kilikuwa; Van Crombrugge, Keita/Milicevic dk74, Luis Garcia, Marreh, Toyokawa/Essende dk68, Blondelle, Gnaka/Schouterden dk82, Pouraliganji, Ocansey na Fall.
  KRC Genk; Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest, Urones, Heynen, Malinovskyi, Pozuelo/Berge dk65, Ndongala/Seigers dk91, Paintsil/Gano dk78 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA APIGA ZOTE MBILI KRC GENK YASHINDA 2-0 UGENINI LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top