• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 27, 2018

  LIVEROOOL YAZIDI 'KUPOTELEA' KILELENI LIGI KUU ENGLAND

  Mshambuliaji Mohamed 'Mo' Salah akishangilia baada ya kuifungia Liverpool bao la pili kwa penalti dakika ya 47 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield. Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Dejan Lovren dakika ya 11, Xherdan Shaqiri dakika ya 79 na Fabinho dakika ya 85 na kwa ushindi huo, kikosi cha kocha Mjerumani Jurgen Klopp kinafikisha pointi 51 baada ya kucheza mechi 19, kikiendelea kuongoza ligi hiyo, kikifuatiwa na Tottenham Hotspur wenye pointi 45 za mechi 19, Manchester City pointi 44 mechi 19, Chelsea pointi 40 mechi 19 na Arsenal wenye pointi 38 za mechi 19 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVEROOOL YAZIDI 'KUPOTELEA' KILELENI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top