• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 24, 2018

  SIMBA PEKEE AFRIKA MASHARIKI NA KATI ILIYOFUZU MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA ni timu pekee ya Afrika Mashariki na Kati iliyofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/2019.
  Hiyo ni baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nkana FC ya Zambia jana jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3, kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Kitwe Jumamosi iliyopita. 
  Kocha Mbelgiji wa Simba SC, Patrick J. Aussems akiwa amemkumbatia mfungaji wa bao la tatu, Mzambia Clatous Chama

  Mbali na Simba SC, timu nyingine zilizofuzu Ligi ya Mabingwa Afrika ni mabingwa watetezi, Esperance na Club Africain zote za Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Ismailia, Al Ahly za Misri.
  Zimo pia TP Mazembe na AS Vita za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Wydad Casablanca ya Morocco, JS Saoura, CS Constantine za Algeria, Horoya FC ya Guinea, Lobi Stars ya Nigeria, FC Platinums ya Zimbabwe na ASEC Mimosa ya Ivory Coast.
  Upangwaji wa makundi na ratiba ya hatua hiyo unatarajiwa Ijumaa wiki hii makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.
  Mara ya mwisho Tanzania kuingiza timu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mwaka 2003 na walikuwa hao hao Simba SC waliofika hatua hiyo, wakifuata nyayo za wapinzani wao wa jadi, Yanga SC waliokuwa timu ya kwanza nchini kufikia mafanikio hayo mwaka 1998. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA PEKEE AFRIKA MASHARIKI NA KATI ILIYOFUZU MAKUNDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top