• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 24, 2018

  JOSHUA MBISSE WA KING’ORI MKOANI ARUSHA AKABIDHIWA BAJAJI YAKE YA SPORTPESA

  IKIWA ni muendelezo wa kukabidhi bajaj za washindi kwenye promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa timu ya ushindi imeendelea kuzunguka huku na kule na kipindi hiki ni zamu ya Jiji la Arusha.
  Hapa anakabidhiwa mshindi wa droo ya Joshua Mbisse wa King’ori Arusha ikiwa ni kutokana na mafanikio ya ubashiri aliouweka kupitia SportPesa Kwa njia ya USSD yani *150*87#
  Akipokea bajaj yake Mbisse aliishukuru SportPesa kwa kumuwezesha kushinda bajaj na hiyo imempa nguvu kubwa na matumaini  ni kubadili maisha na kufungua wigo mpya atakaomuwezesha kuinuka kiuchumi.
  "Sasa nimeamini mchezo huu wa ubashiri kutoka SportPesa ni wa uhakika na hauna longolongo kama nilivyokuwa nikifikiri, Ghafra ushindi wangu umenifanya nibadili fikra tofauti na mtazamo wa hapo awali, mambo ni mengi ya kufanya kupitia bajaj hii nachokiona kikubwa ni kutengeneza maisha yangu Na kuyaboresha Kabisa sina budi kushukuru kwa hili"
  Joshua Mbisse wa King’ori mkoani Arusha baada ya kukabidhiwa Bajaji yake  
  Mkakati mwingine mkubwa ni kumalizia ujenzi wa nyumba yake ambayo mpaka hivi sasa ujenzi ulikuwa haujamalizika.
  Ushindi wa Mbisse ulipokelewa kwa Furaha kubwa na wanakijiji wenzake Wengi wao wakiamini kuwa mafanikio ya Mshindi huyo ni ya kwako pia maana bajaj hiyo inaweza kuwa msaada hata kwa upande wao kwenye masuala ya usafiri 
  Mbali ya kushinda bajaj SportPesa inakukumbusha kucheza jackpot ambayo imesimamia kwenye zaidi ya sh.  Milioni 420 hii inampa mtu nafasi ya kubashiri Mechi 13 na akifanikiwa kuzibashiri mechi zote kwa usahihi ataondoka nazo zote lakini yule anayefanikiwa kubashiri Mechi 10, 11, na 12 kwa ufasaha anaondoka na bonus ambayo ni ya utofauti na wala haigawanyiki.
  Katika msimu huu wa sikukuu wateja wa mitandao yote ya simu wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka SportPesa kama Bajaji, Jezi za Simba na Yanga, Smartphone(simu janja) pamoja na safari ya kwenda kushuhudia ligi kubwa mbili suniani yaani Hispania na Uingereza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JOSHUA MBISSE WA KING’ORI MKOANI ARUSHA AKABIDHIWA BAJAJI YAKE YA SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top