• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 28, 2018

  AFRIKA MASHARIKI YAPEWA VIGOGO KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU za Afrika Mashariki, Gor Mahia ya Kenya, Vipers SC na KCCA ya Uganda zimepangiwa wapinzani wagumu katika mechi za mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Katika droo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri Gor Mahia itamenyana na New Star ya Cameroon, Vipers na CS Sfaxien ya Tunisia na KCCA na AS Otoho ya Kongo.
  Al Hilal ya Sudan itamenyana na mwanachama mwenzake wa CECAFA, Mukura Victory ya Rwanda, wakati beki Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy timu yake, Nkana FC ya Zambai itamenyana na FC San Pedro ya Ivory Coast.
  Vigogo wa Misri, Zamalek watamenyana na wababe wenzao wa Morocco, Ittihad Tanger ambao ndugu zao, Raja Casablanca watamenyana na African Stars ya Namibia. 
  Washindi 15 wataungana na Etoile du Sahel ya Tunisa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Janauri hadi Machi. 
  Hassan Kessy (kushoto walioinama) timu yake Nkana FC itamenyana na FC San Pedro ya Ivory Coast 

  RATIBA KAMILI MCHUJO WA KUWANIA KUCHEZA 
  HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
  Gor Mahia (Kenya) v New Star (Cameroon)
  Al Ahly Benghazi (Libya) v NA Hussein Dey (Algeria)
  Al Hilal (Sudan) v Mukura Victory (Rwanda)
  Nkana (Zambia) v FC San Pedro (Ivory Coast)
  Coton Sport (Cameroon) v Asante Kotoko (Ghana)
  Zesco Utd (Zambia) v Kaizer Chiefs (Afrika Kusini)
  Stade Malien (Mali) v Petro Atletico (Angola)
  Raja Casablanca (Morocco) v African Stars (Namibia)
  Renaissance Berkane (Morocco) v ASC Jaraaf (Senegal)
  CS Sfaxien (Tunisia) v Vipers SC (Uganda)
  Zamalek (Misri) v Ittihad Tanger (Morocco)
  KCCA (Uganda) v AS Otoho (Kongo)
  Bantu (Lesotho) v Enugu Rangers (Nigeria) 
  Al Nasr (Libya) v Salitas (Burkina Fasso)
  Jimma Aba Jifar (Ethiopia) v Hassania Agadir (Morocco)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AFRIKA MASHARIKI YAPEWA VIGOGO KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top