• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 23, 2018

  NDANDA, MWADUI NA MBAO FC ZATUPWA NJE NA TIMU ZA ‘MCHANGANI’ KOMBE LA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  HATUA ya 64 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) imeendelea leo ikishuhudiwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara zikiendelea kupukutishwa baada ya leo timu tatu kuondolewa na kufanya jumla ya timu hizo kuwa tano hadi sasa.
  Timu zilizoondolewa leo ni Mwadui FC ambao wamefungwa mabao 3-1 na Pan Africa, Ndanda SC wamefungwa na Trans Camp kwa penati 3-2 baada ya kutoka suluhu katika dakika dakika 90, huku Mbao FC wakifungwa na Dar City kwa penati 4-2 baada ya sare ya bao 1-1.
  Timu hizo sasa zinaungana na Tanzania Prisons pamoja na Ruvu Shooting zilizofungashiwa virago jana.
  Mechi nyingine Lipuli FC imeibuka na ushindi wa 9-0 dhidi ya Laela FC, Singida United imeichapa 2-0 Arusha FC, Kagera Sugar imeshinda 2-1 dhidi ya Kumuyanga ugenini na Friends Rangers imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Sharp Striker.
  Nayo Rhino Rangers imeshinda 3-1 dhidi ya Nyamongo, Namungo FC imeichapa 3-0 Sahare All Stars, Reha FC imesonga mbele kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 na Zakhiem FC, Majimaji FC imeichapa 1-0 Gipco FC, Boma FC imeifunga 2-0 Njombe Mji, Cosmopolitan imeitoa Green Warriors kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 na Polisi Tanzania imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Forest FC. 
  Timu zilizofuzu leo ni Dar City, Lipuli FC, Singida United, Trans Camp, Pan African, Kagera Sugar, Friends Rangers, Rhino Rangers, Namungo FC, Reha FC, Majimaji FC, Boma FC, Cosmopolitan na Polisi Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDANDA, MWADUI NA MBAO FC ZATUPWA NJE NA TIMU ZA ‘MCHANGANI’ KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top