• HABARI MPYA

  Sunday, December 30, 2018

  POGBA APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA BOURNEMOUTH 4-1

  Paul Pogba akishangilia baada ya kuifungia Manchester United mabao mawili dakika ya tano na 33 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya AFC Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield. Mabao mengine ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 45 na Romelu Lukaku dakika ya 72, wakati la AFC Bournemouth limefungwa Nathan Ake dakika ya 45 na ushei.
  Na kwa ushindi huo wa tatu mfululizo tangu timu hiyo na kocha wake, Jose Mourinho na kuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer, Manchester United inafikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 20, ingawa inaendelea kushika nafasi ya sita nyuma ya Arsenal yenye pointi 38 za mechi 20 pia      
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POGBA APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA BOURNEMOUTH 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top