• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 17, 2018

  NI AZAM NA MADINI FC NA YANGA SC KUKUTANA NA TUKUYU STARS KATIKA KOMBE LA TFF MWISHONI MWA WIKI DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC itamenyana na Madini FC katika hatua ya 64 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), wakati Yanga itamenyana na Tukuyu Stars ‘Banyambala’.
  Hiyo ni baada ya jana Madini FC kuitoa Stand Babati kwa kuichapa mabao 5-1 na Tukuyu Stars kuitoa Ihefu, zote za Mbeya kwa penalti 5-4 kufuatia satre ya 1-1.
  Ikumbukwe kwenye droo ya raundi ya tatu ya michuano hiyo, iliyofanyika wiki iliyopita makao makuu ya Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam Simba SC watakuwa wenyeji wa Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma.

  Mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wao wataanza na Mtibwa Sugar na Kiluvya United ya Pwani Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, wakati washindi wa pili Singida United wataanzia nyumbani pia Uwanja wa Namfua mkoani Singida dhidi ya Arusha FC. 
  Mechi zitachezwa wikiendi ijayo kuanzia Desemba 21 hadi 24 na hii moja kwa moja inamaanisha mechi itachezwa kabla au baada ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Nkana FC ya Zambia Desemba 23 mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI AZAM NA MADINI FC NA YANGA SC KUKUTANA NA TUKUYU STARS KATIKA KOMBE LA TFF MWISHONI MWA WIKI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top