• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 22, 2018

  CHILUNDA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA TENERIFE KUPATA SARE MBELE YA GRANADA

  Na Mwandishi Wetu, TENERIFE
  MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania Shaaban Iddi Chilunda jana alitokea benchi dakika 10 aa mwisho timu yake, Tenerife ikilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Granada katika mchezo wa Ligi Daraja kwa Kwanza Hispania.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez mjini Santa Cruz de Tenerife, Chilunda aliingia wakati timu yake ipo nyuma kwa bao la Antonio Puertas aliyefunga dakika ya 10.
  Na baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Iker Undabarrena dakika ya 81, Chilunda akaisaidia timu yake kusawzisha bao kupitia kwa Joao Rodriguez aliyefunga dakika ya 90+2.

  Kwa matokeo hayo, Tenerife imejiongezea pointi moja na kufikisha 19 katika mechi ya 19, ingawa nafasi ya 17 katika Segunda inayoshirikisha timu 22.
  Granada yenyewe inazidi kujiweka katika mazingira ya kurejea La Liga, ikifikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 19, hivyo kuendelea kuongoza Segunda kwa pointi tatu zaidi ya Deportivo La Coruna walio nafasi ya pili.
  Jana Chilunda amecheza mechi ya tatu tu tangu asajiliwe Tenerife kwa mkopo kutoka Azam FC Agosti mwaka huu na zote akiingia dakika 10 za mwisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHILUNDA ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA TENERIFE KUPATA SARE MBELE YA GRANADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top