• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 17, 2018

  MAN UNITED YAPEWA PSG 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA

  TIMU ya Manchester United itamenyana na Paris Saint-Germain katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Timu nyingine tatu za England nazo zimepangiwa wapinzani wagumu kutoka Ujerumani katika hatua hiyo.
  Liverpool imepangiwa Bayern Munich, wakati Manchester City itamenyana na Schalke na Tottenham Hotspur imepewa Borussia Dortmund.
  Kikosi cha Jose Mourinho kinachosuasua kitaanzi nyumbani Uwanja wa Old Trafford kabla ya kusafiri kuwafuata matajiri wa Ufaransa kwa mchezo wa marudiano.


  RATIBA KAMILI HATUA YA 16 BORA YA LIGI YA MABINGWA UKAYA

  Schalke vs Manchester City
  Atletico Madrid vs Juventus
  Manchester United vs PSG
  Tottenham vs Borussia Dortmund 
  Lyon vs Barcelona
  Roma vs Porto 
  Ajax vs Real Madrid
  Liverpool vs Bayern 

  Man City, timu pekee ya England iliyoongoza kundi, itaanzia ugenini kabla ya kucheza nyumbani mechi ya marudiano, lakini timu nyingine zitaanzia ugenini.
  Mechi za kwanza zitachezwa Februari 12, 13, 19 na 20 na za marudiano zitachezwa Machi 5, 6, 12 na 13 mwaka 2019.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAPEWA PSG 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top