• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 30, 2018

  MAN CITY YAZINDUKA NA KUICHAPA SOUTHAMPTON 3-1

  Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia Manchester City bao la tatu dakika ya 45 na ushei katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton Uwanja wa St. Mary's leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England. Mabao mengine ya Man City yamefungwa na David Silva dakika ya 10 na James Ward-Prowse aliyejifunga dakika ya 45, wakati la Southampton limefungwa na Pierre-Emile Hojbjerg dakika ya 37.
  Kwa ushindi huo ikitoka kufungwa mechi mbili mfululizo, Man City inafikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 20 na sasa inarejea nafasi ya pili, nyuma ya Liverpool yenye pointi 54 za mechi 20 pia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAZINDUKA NA KUICHAPA SOUTHAMPTON 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top