• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 18, 2018

  SAMATTA: HATUTAICHUKULIA POA SLAVIA PRAHA, KATIKA MICHUANO YA EUROPA LEAGUE HAKUNA TIMU YA KUBEZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mtanzania Mbwana Ally Samatta amesema kwamba hawataidharau Slavia Praha ya Jamhuri ya Czech waliyopangwa nayo katika hatua ya 32 ya michuano ya Europa League.
  “Hakuna timu ya kubeza katika mashindano hayo, tutajiandaa vyema kukabiliana nayo, lengo letu ni kufika mbali ikibidi kuchukua hadi Kombe,”amesema Samatta alipozungumza na Bin Zubeiry Sports – Online mapema leo.
  Pamoja na KRC Genk kupangiwa S.K. Slavia Praha ya Jamhuri ya Czech, katika hatua ya 32 ya Europa League baada ya droo iliyopangwa jana mjini Nyon, Uswisi timu za England, Arsenal na Chelsea nazo zimepata wapinzani hafifu kidogo.
  Mbwana Samatta atakutana na Slavia Praha ya Jamhuri ya Czech katika hatua ya 32 ya Europa League


  RATIBA HATUA YA 32 BORA MICHUANO YA EUROPA LEAGUE

  Viktoria Plzen vs Dinamo Zagreb
  Brugge vs Salzburg
  Rapid Vienna vs Inter Milan 
  Slavia Prague vs Genk
  Krasnodar vs Bayer Leverkusen
  Zurich vs Napoli 
  Malmo vs Chelsea 
  Shakhtar Donetsk vs Eintracht Frankfurt  
  Celtic vs Valencia 
  Rennes vs Real Betis 
  Olympiacos vs Dinamo Kiev 
  Lazio vs Sevilla 
  Fenerbahce vs Zenit St Petersburg
  Sporting Lisbon vs Villarreal
  BATE Borisov vs Arsenal 
  Galatasaray vs Benfica   Arsenal itamenyana na BATE Borisov na Chelsea itamenyana na Malmo ya Sweden, wakati mabingwa wa Scotland, Celtic wamepangiwa wapinzani wagumu katika hatua hii ya kwanza ya mtoano, ambao ni Valencia, ambao wameporomoka kutoka Ligi ya Mabingwa.   
  Mechi nyingine za hatua hiyo Lazio, inayoshika nafasi ya tano katika Serie A, inakutana na mabingwa mara tano, Sevilla na Galatasaray watamenyana na Benfica. 
  Mechi za kwanza zitachezwa Februari 12 na 14 na za marudiano zitafuatia Februari 20 na 21 mwakani.
  Samatta alijiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na hadi sasa amekwishacheza mechi 134 katika mashindano yote na amefunga mabao 53.
  Katika Europa League Samatta amecheza mechi 22 na kufunga mabao 14, wakati katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 104 na kufunga mabao 38 na Kombe la Ubelgiji mechi nane na kufunga mabao mawili tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA: HATUTAICHUKULIA POA SLAVIA PRAHA, KATIKA MICHUANO YA EUROPA LEAGUE HAKUNA TIMU YA KUBEZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top